NISHA ASHINDWA KUKAA KIMYA KUHUSU SKENDO YA KUTOA MIMBA INAYOMKABILI, AAMUA KUFUNGUKA HAYAAAA. SOMA HAPA

MTAYARISHAJI na mwigizaji wa Bongo Movie, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka
akidai kuwa maendeleo yake katika filamu yamemtengenezea maadui.
Akizungumza na Mwanaspoti, Nisha alisema maadui hao wamefikia hatua ya
kumzushia kuwa ametoa mimba au ‘ame-flush’ wakati anaumwa na kichwa.
Alisema amebaini kuwa ana maadui wengi ambao hawapendi kuona
anavyoendelea na ndio maana wamekuwa wakimzushia maneno yanayomchafua
katika jamii.
“Huku Bongo Movie hatari sana, hata ukiwa na rafiki yako kuwa makini
naye kwani ipo siku atakuuza na kukupoteza, mimi sifuatilii mambo ya mtu
mwingine zaidi ya biashara zangu na kazi yangu tu,’’ alisema.
“Bongo Movie kuna watu wanaotaka kila siku wajue Nisha kafanya nini ili
wakuseme vibaya, kuwa na maendeleo ni kutengeneza maadui nahisi kuwa na
maadui pembeni yangu,” aliongeza Nisha.
Nisha ambaye hivi karibuni alikuwa mgonjwa, alitoa kauli hiyo baada ya
kuripotiwa maradhi yaliyokuwa yakimsibu chanzo chake ni mimba aliyoitoa.
Hata hivyo Nisha aliwashangaa waliomzushia hilo na kufafanua kuwa
alikuwa anaumwa kichwa na kama ingekuwa ametoa mimba angekuwa anaumwa
tumbo.
0 comments: