BannerFans.com

HATARI:KAJALI ALISHWA SUMU, AKIMBIZWA HOSPITALINI

1 comments

Mwanadada mwigizaji Kajala juzi alikumbwa na dhahama ya kusikitisha baada ya kulishwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni sumu alipokuwa kwenye show ya msanii wa muziki kizazi kipya Izzo Business huko.

Akielezea Zaidi kajala alisema…

‘’Jana (juzi) nilivyokuwa kwenye shoo ya izzo ghafla nikaanza kuumwa nikapelekwa home halafu nikaenda hospitali. Nilivyo pimwa nikakutwa nimekunywa kitu chenye sumu lakini namshukuru mungu naendelea vizuri asante mungu kwa kila jambo...

Hali ya kajala ni nzuri na ameruhusiwa kutoka hospitalini sasa. Pole sana Kajala

HATARI:KAJALI ALISHWA SUMU, AKIMBIZWA HOSPITALINI

0 comments


Mwanadada mwigizaji Kajala juzi alikumbwa na dhahama ya kusikitisha baada ya kulishwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni sumu alipokuwa kwenye show ya msanii wa muziki kizazi kipya Izzo Business huko.

Akielezea Zaidi kajala alisema…

‘’Jana (juzi) nilivyokuwa kwenye shoo ya izzo ghafla nikaanza kuumwa nikapelekwa home halafu nikaenda hospitali. Nilivyo pimwa nikakutwa nimekunywa kitu chenye sumu lakini namshukuru mungu naendelea vizuri asante mungu kwa kila jambo...

Hali ya kajala ni nzuri na ameruhusiwa kutoka hospitalini sasa. Pole sana Kajala

VAI WA UKWELI: TAMAA YA FEDHA ILINIPONZA, NAJUTA

0 comments


SIKU chache baada ya msanii anayekuja kwa kasi kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ kuingia kwenye kumi na nane za mtego wa kujiuza wa kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’, ameibuka na kusema, anajuta, amekoma na hatarudia tena.

Habari ya Vai kunaswa katika mtego wa kujiuza iliripotiwa na gazeti damu moja na hili, Ijumaa toleo la wiki iliyopita, ambapo msanii huyo aliingia mkenge baada ya kukubali kukutana na ‘pedeshee’ mmoja kutoka mkoani kwa lengo la kumpa uroda kwa malipo ya shilingi 500,000.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko juzi, Jumatatu jijini Dar es Salaam, Vai alisema: “Kiukweli lile tukio lilinichanganya sana lakini pia limenipa fundisho kubwa. Nawaomba ndugu zangu na mashabiki wangu wote wanisamehe kwa dhati kabisa.

“Naahidi sitarudia tena ujinga kama ule. Ilikuwa ni tamaa tu. Hivi ninavyozungumza na wewe nipo kwa editor (mhariri) nasimamia editing (uhariri) ya filamu yangu ambayo ipo katika hatua za mwisho kuingia mitaani. Niko bize na kazi, acha niwekeze kwenye ujasiriamali tu. Nawashauri wasanii wenzangu tutulie maana OFM wapo macho.”

Alisema, katika filamu yake hiyo aliyoipa jina la Beautiful Liar amewashirikisha wakongwe Mohammed Fungafunga ‘Jengua’, Hashim Kambi ‘Wingo’ na mastaa wengine kwenye tasnia hiyo na kwamba mashabiki wake wakae mkao wa kula.
Kuomba msamaha ni uungwana, ikiwa Vai umeona kosa lako na kuomba radhi ni jambo zuri la kupongezwa. Tunakutakia kila la heri katika mabadiliko hayo, tukikusisitiza iwe kweli maana OFM bado ipo kazini. – MHARIRI.

Credits:Global Publishers

AGNESS MASOGANGE AWAPAGAWISHA WAKAZI WA DODOMA KWA MAUNO YAKE-DOLA ZAMWAGWA

0 comments



Agness masogange alikuwa kivutio kikubwa pale walipokuwa wakicheza kwenye uzinduzi wa Pub Moja huko Mjini Dodoma..Mapendeshee wa huko walimwaga dola kama njugu kufurahia alichokuwa anafanya Agness Jukwaani kwa kukata Mauno..

HATIMAYE HUDDAH MONROE AMTAJA MPENZI WAKE MPYA..HUYU HAPA

0 comments


Aliyekuwa mwakilishi wa Kenya katika jumba la Big Brother msimu uliopita, Huddah Monroe ambaye pia alikuwa mpenzi wa rapper Prezzo, ametangaza kuwa kwenye penzi jipya na msanii mwingine wa Kenya aitwae Colonel Mustafa.

TUKIO KATIKA PICHA AJALI MBAYA YATOKEA MIKESE MOROGORO LEO ASUBUHI

0 comments


 Ankle habari. Leo asubuhi eneo la Mikese, Morogoro, tumekutana na na ajali  mbaya sana ya magari mawili, moja la mafuta, kugongana uso kwa uso na kutumbukia mtaroni na yote kushika moto. Inasadikiwa mtu mmoja ambaye ni dereva wa magari hayo kateketea kabisa kwa moto. Picha na Mdau Sixmund

 Hakuna cha kufanyika kutokana na moto mkubwa na moshi mwingi wakati magari hayo yakiteketea
 Mlipuko mkubwa wakati matenki ya mafuta yakilipuka
Askari wa kikosi cha zimamoto wakijaribu kuuzima moto huo

WATOTO WALIO ZALIWA WAMEUNGANA WAREJEA DAR BAADA YA KUTENGENISHWA

0 comments

Watoto pacha, Elikana na Eliud waliokuwa wameungana wamerejea nchini jana wakitokea India walipokuwa kwa ajili ya kutenganishwa, tayari kwa kusherehekea kumbukumbu yao ya kutimiza mwaka mmoja leo.

Waliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa 10:30 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Oman, wakiwa na mama yao, Grace Joel (20) ambaye muda wote alionekana mwenye furaha.

Elikana na Eliud walizaliwa Februari 20, mwaka jana wilayani Kyela, Mbeya wakiwa wameungana na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambako walipata rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Juni mwaka jana, Serikali iliwapeleka Hospitali ya Chennai, India ambako Desemba 16, mwaka jana walifanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha.

Akizungumza baada ya kutua jana, Grace alisema: “Nina furaha ya ajabu, sijui nimshukuru vipi huyu Mungu wangu, ni mkuu mno. Ninawashukuru sana madaktari wa India, ninawashukuru madaktari wa Muhimbili na sana naishukuru Serikali yangu kwa kunipa msaada huu mkubwa. Siamini kama leo ningekuwa narudi salama na watoto wangu kila mmoja akijitegemea,” alisema Grace.

“Kesho (leo) ni birthday yao, wanatimiza mwaka mmoja, ni furaha ya ajabu niliyo nayo, siwezi kuelezea. Siku nilipoambiwa watoto wangu watafanyiwa upasuaji mkubwa na watapumulia mashine kwa wiki moja, nilichanganyikiwa kwa kweli, sikutamani tena hata hiyo operesheni ifanyike ila sikuwa na jinsi zaidi ya kumwomba Mungu.”

Akizungumza uwanjani hapo, Dk Glory Joseph kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando ambaye aliongozana na watoto hao kurudi nchini alisema: “Watoto wamerejea salama na wanaendelea vizuri ila watakuwa Moi (Hospitali ya Mifupa Muhimbili), kwa uangalizi maalumu mpaka hapo madaktari watakapoona inafaa ndipo watapewa ruhusu ya kurudi nyumbani kwao Mbeya.

“Agosti watarudishwa tena India kwa ajili ya upasuaji katika njia ya mkojo na kufunga sehemu ya utumbo,” alisema.

Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja alisema upasuaji wa watoto hao ulichukua saa 18. Katika muda huo, saa 13 zilitumika kutenganisha viungo vilivyoungana sehemu ya chini ya uti wa mgongo, sehemu ya utumbo mpana, njia ya mkojo, kibofu na sehemu ya uume, wakati saa tano zilitumika kuunganisha sehemu zilizotenganishwa.

Pacha hao walifanyiwa upasuaji na madaktari 20 na wataalamu wengine wa afya ambao walitumia saa 18 kuwatenganisha. Kiasi cha Sh100 milioni kilitumika.

Meneja wa Huduma za Wagonjwa wa Kimataifa wa hospitali hiyo, Senu Sam alizungumza na gazeti dada la Mwananchi, The Citizen juzi na kusema wamefanya sherehe kwa ajili ya mafanikio ya upasuaji huo.

Sam alisema pacha hao wameonana ana kwa ana kwa mara ya kwanza, wiki tatu baada ya upasuaji... “Imekuwa faraja kuwaona wakitazamana. Eliudi alivishika vidole vya mkono wa Elikana na kuvichezea. Wanaonekana kufurahia mazingira mapya,” alisema Sam.